Pages

Monday, December 22, 2014

KIU Ufunguzi wa tawi kwa ufupi

Tarehe 19/12/2014 ulifanyika mkuta noa wa wanafunzi wa fani ya maabara tiba katika chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala. kilichopo eneo la Gongo la mboto jijini Dar es salaam

Zifuatazo ni picha za matukio mbali mbali
 Raisi wa TAMELASA taifa akitoa historia ya chama kwa wanafunzi
 Sehemu ya wanafunzi wa KIU wakifuatilia maeleza ya viongozi wa TAMELASA taifa

Mkutano singida

 Mkutano na wanafunzi na wanajumuiya ya wanafunzi wa maabara katika chuo cha maabara singida

Mkutano KAM College

Raisi wa TAMELASA taifa akielezea historia ya TAMELASA kwa wanafunzi wa fani ya maabara tiba katika chuo cha KAM kilichopo Kimara Dar es salaam

 Sehemu ya wanafunzi wa maabara waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa ukaribu maelezo kutoka kwa viongozi wao

MUHAS wakaribisha First Year

Sherehe ya kuwakaribisha mwaka wa kwanza Muhimbili ilifanyika jumamosi ya tarehe 20/12/2014
 Kamati ya maandalizi ya sherehe wakijitambulisha mbele ya wageni na wanajumuiya wote
 Mgeni rasmi Ng Kweka kwaniaba ya mkuu school of medical Laboratory akisalimia wanafunzi
 Mgeni rasmi Ng Kweka ambaye pia ni mwenyekiti wa MeLSAT tawi la Muhimbili akisisitiza jambo alipokuwa akielezea umuhimu na uzuri wa fani ya maabara, kulia kwake ni raisi wa chama cha wanafunzi wa fani ya maabara tiba Tanzania Ng Ambele Eliah

 High table ikifuatilia kwa umakini hutuba ya mgeni rasmi kushoto kabisa aliyevaa gauni la njano ni mwakilishi wa wanafunzi wa fani ya maabara Muhimbili (SR)
 Waandaaji wakijitambulisha


 Raisi wa chama cha wanafunzi wa fani ya maabara tiba Tanzania akielezea historia ya chama TAMELASA nchini

Friday, November 28, 2014

Taarifa kwa ufupi

Tuna kila sababu ya kufurahia weekend 

1....>. 
Idadi ya wanafunzi wa maabara wanaopata mikopo na/au udhamini katika masomo yao kuanzia ngazi ya cheti mpaka degree inazidi kuchanja mbuga. Ni swala la kujipongeza maana hivi vitu haviji kienyeji tu ni kazi imefanyika na inaendelea kufanyika namshukuru Mungu, na wote walio jitolea bega kwa bega katika kufanikisha hili.. Safari inaendelea tutafika NITAWALETEA TAARIFA NA RIPOTI KAMILI. kuna mambo nayaweka sawa, kwanza nionane na hawa wakubwa.

2.....>
Kiapo cha Wanafunzi ninacho mkononi nategemea ushirikiano kutoka kwa viongozi wa vyuo vikuu vyote ili ikiwezekana mwaka huu kiweze kutumika. Naomba yeyote anaye soma taarifa hii ajaribu kuifikisha kwa wanafunzi waliomaliza mwaka huu ili tusaidiane kwa hilo maana najua ratiba za maafali mengi tayari zimepangwa.

Maoni na ushauri
Namba yangu ipo wazi mchana na jioni zote isipokuwa ni vizuri ukaandika sms kama sijabanwa sana tunaweza ongea lakini nitakujulisha maana naweza kuwa darasani. 
0716078422 na 0762170454

WEEKEND NJEMA
Ambele Eliah
President


Wednesday, November 26, 2014

Softy Trainer's training on 22 to 23 nov2014

Training ya ujasiliamali na uwajibikaji kazini ilifanyika katika vyuo vya MUHAS na IMTU siku ya jumamosi na jumapili tarehe 22 na 23 mwezi November 2014. Siku ya kwanza mafunzo yalifanyika tofauti lakini siku ya pili wanafunzi wa Muhimbili na IMTU walifanya mafunzo pamoja katika chuo kikuu cha MUHAS. Tujikumbushe baadhi ya matukio
 Baadhi ya wanafunzi wa IMTU walio hudhuria mafunzo ya Ujasiliamali jumamosi (wawekezaji na matajiri wa kesho)

Wednesday, November 12, 2014

CUHAS-BUGANDO matukio jioni 2

Nitaendelea kuweka picha zaidi


CUHAS-BUGANDO matukio jioni-1

 Walitokelezeajeeeeeee!

CUHAS-BUGANDO matukio 4

Nimechoka kuandika angalia picha tu zinazungumza zenyewe

CUHAS-BUGANDO matukio - 3


CUHAS-BUGANGO matukio 2

Ilikuwa ni Shedaaaaa.
HONGERENI SANA (watoto wa baba paroko)

 Kuku aliye karibia kuwatoa roho wanafunzi... maana ilikuwa ukimkamata wakooooo, watu walisha nunua vitunguu ilikuwa shedaaa
 Kuku kuku kuku

CUHAS -BUGANDO matukio



KWANZA KABISA  NAPENDA  KUCHUKUA  NAFASI  HII  KUWAPONGEZA  WANA TAMELASA CUHAS –BUGANDO MWANZA PAMOJA NA WADAU  WOTE  KWA  KUONESHA KUWA  HAKUNA  KINACHOSHINDIKANA PALIPO  NA  NIA MOJA. KIPEKEE  NAUPONGEZA  UONGOZI  WA  TAMELASA-CUHAS  CHINI  YA  MWENYEKITI  WA TAWI  NDUGU, ALPHONCE CHARLES
I’ M  PROUD OF  YOU  DUDES
AMBELE   ALIAH
PRESIDENT
……………………………………………………………….
Katika kuwakaribisha  wanafunzi  wa mwaka wa kwanza  wa Degree na Diploma za maabara tiba katika chuo kikuu cha CUHAS –BUGANDO wana TAMELASA wamefanya tamasha kubwa na BONANZA tar 08/11/2014 likifuatiwa na tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Gold city hapa jijini Mwanza  tafrija  hiyo  pamoja  na  mabo  mengine  iliambatana  na  tukio  kutunisha  mfuko  wa  tawi  (FUND RISING) ambapo  pesa  taslim na ahadi zilizotolewa  ziliweza  kufikia  lengo  na zaidi. Mimi mwenyewe Mr President  nilikuwepo kushuhudia maandalizi ya mwisho na jinsi walivyoendesha zoezi zima. Nitawaletea  baadhi  ya  matukio  yaliyojiri  oneni  uhondo  ilikuwa Nishedaaaa


BONANZA
Kulikuwa na michezo mbalimbali ambayo ilileta raha na kuifanya siku iwe ya kukumbukwa

1. kukuimbia na Gunia
2. Riadha mita 100
3. kufukuza kuku
4. shindano la kula
5. kufukuza kuku na 
6. mpira wa miguu
 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia Bonza hilo wengine wakisubiri muda wa mchezo wanaoupenda wapate kushiriki


Wednesday, November 5, 2014

Picha za viongozi wa TAMELASA eastern zone

 Baadhi ya viongozi wa TAMELASA wakipiga picha baada ya kumaliza mkutano wao siku ya Jumamosi 1/11/2014 kutoka kushoto ni Magdalena (makamu mwenyekiti IMTU), Eliza (katibu IMTU), Ernest (mwenyekiti MUHAS) na Magonyozi(mwenyekiti IMTU)

NTA levels na mtaala mpya



Leo hii tarehe 05/11/2014 nimetoka ofisi ya mkurugenzi mafunzo nilikuwa na maswali machache ambayo nilitaka kupewa ufafanuzi ili niweze kuelewa na niweze kuwataarifu, kujibu au kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali ambayo nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na wanachama leo nitafafanua jambo moja tu sababu ya muda
1.      Nilitaka kujua  kuhusiana na mtaala mpya ambao umepitishwa na unaanza kutumika kwenye vyuo vyetu vya afya za binadamu. Mtaala mpya unaanza kutumika rasmi kwa levels zote
Kabla sijaendelea zaidi ningependa niwakumbushe kidogo hizi NTA levels. NTA ni kifupisho cha maneno National Technical Award.   Levels 1,2 na 3 zinatumika  VETA na huwa zinaandikwa NVTA. Kwa kada zote za afya tunaanza na NTA level 4. Ukisoma Level  4 na 5 unapata certificate (Laboratory assistant au Clinical Assistant) ukifaulu na GPA nzuri unaruhusiwa kuendelea na NTA level 6 moja kwa moja (Ordinary Diploma)la unakwenda kazini baadae utakwenda kusoma diploma 

Wednesday, October 29, 2014

Tangazo -Eastern Zone



Kutakuwa na mkutano wa viongozi wote wa matawi ya TAMELASA  kanda ya mashariki.

Mahali                  :               Muhimbili  MTC  Hostel
Washiriki              :               Viongozi wa matawi i.e. Mwenyekiti, katibu na Mhazini
Muda                    :               kuanzia saa 2:00 (mbili kamili) asubuhi

Saturday, October 25, 2014

Vifaa vya kubaini dalili za Ebola

VIFAA VYA KUBAINI DALILI ZA AWALI ZA UGONJWA WA EBOLA KUPITIA JOTO LA MWILI

 

Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi Dkt. Elias
Chinamo moja ya kifaa (kamera) itakayotumika kupima dalili za ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.

Thursday, October 23, 2014

more 2013 pictures

matukio zaidi ya mwaka 2013

Picha zaidi za 2013

Tujikumbushe zaidi

2013 events your comment

Tukutanapo haijalishi ni kwa tukio gani inakuwa raha saaana... Hebu tujikubushe

Matukio yaliyopita

Wiki ya maabara Tanzania. wanafunzi wa maabara za afya ambao ni wanachama wa TAMELASA wakishiriki wiki ya maabara (Laboratory week) pamoja na wafanyakazi wa maabara ambao ni wanachama wa MeLSAT


St.Aggrey event 15/10/2014

Wanafunzi wa chuo cha maabara St.Aggrey kilichopo Mbeya wakisikiliza maelezo ya kina kutoka kwa viongozi kabla ya kufunguliwa tawi la TAMELASA (Tanzania Medical Laboratory Students Association) chuoni kwao 15/10/2014

Mt.Ukombozi wakiagana

Wanafunzi wa chuo cha Mount Ukombozi Heath Sciences Training Centre. waliandaa sherehe fupi kuwaaga wenzao mnamo 03/10/2014
 Rais wa chama cha wafanyakazi wa Maabara Tanzania Ndugu Mrina (katikati) akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa fani ya maabara ngazi ya cheti kushotokwake ni Raisi wa chama cha wanafunzi wa fani ya maabara Tanzania Ndugu Ambele Eliah

Wednesday, October 22, 2014

Mbalizi na St Aggrey wapata viongozi

Matawi mapya ya TAMELASA katika vyuo vya Mbalizi na St Aggrey yamefanya uchaguzi na kupata viongozi wao wa kwanza wa matawi hayo.

MBALIZI viongozi ni:

Friday, October 17, 2014

RUCO event

Picha chini. Wanafunzi wa  fani ya maabara chuo cha RUCO Iringa wakifuatilia maelezo kutoka kwa rais wa TAMELASA Tanzania October 9, 2014 



NEW BRANCHES

Two new branches of TAMELASA has been launched in Mbeya this October. The branches are from Mbalizi and St. Aggrey schools of medical laboratory.For more information keep on visiting this site.