Pages

Friday, November 28, 2014

Taarifa kwa ufupi

Tuna kila sababu ya kufurahia weekend 

1....>. 
Idadi ya wanafunzi wa maabara wanaopata mikopo na/au udhamini katika masomo yao kuanzia ngazi ya cheti mpaka degree inazidi kuchanja mbuga. Ni swala la kujipongeza maana hivi vitu haviji kienyeji tu ni kazi imefanyika na inaendelea kufanyika namshukuru Mungu, na wote walio jitolea bega kwa bega katika kufanikisha hili.. Safari inaendelea tutafika NITAWALETEA TAARIFA NA RIPOTI KAMILI. kuna mambo nayaweka sawa, kwanza nionane na hawa wakubwa.

2.....>
Kiapo cha Wanafunzi ninacho mkononi nategemea ushirikiano kutoka kwa viongozi wa vyuo vikuu vyote ili ikiwezekana mwaka huu kiweze kutumika. Naomba yeyote anaye soma taarifa hii ajaribu kuifikisha kwa wanafunzi waliomaliza mwaka huu ili tusaidiane kwa hilo maana najua ratiba za maafali mengi tayari zimepangwa.

Maoni na ushauri
Namba yangu ipo wazi mchana na jioni zote isipokuwa ni vizuri ukaandika sms kama sijabanwa sana tunaweza ongea lakini nitakujulisha maana naweza kuwa darasani. 
0716078422 na 0762170454

WEEKEND NJEMA
Ambele Eliah
President


Wednesday, November 26, 2014

Softy Trainer's training on 22 to 23 nov2014

Training ya ujasiliamali na uwajibikaji kazini ilifanyika katika vyuo vya MUHAS na IMTU siku ya jumamosi na jumapili tarehe 22 na 23 mwezi November 2014. Siku ya kwanza mafunzo yalifanyika tofauti lakini siku ya pili wanafunzi wa Muhimbili na IMTU walifanya mafunzo pamoja katika chuo kikuu cha MUHAS. Tujikumbushe baadhi ya matukio
 Baadhi ya wanafunzi wa IMTU walio hudhuria mafunzo ya Ujasiliamali jumamosi (wawekezaji na matajiri wa kesho)

Wednesday, November 12, 2014

CUHAS-BUGANDO matukio jioni 2

Nitaendelea kuweka picha zaidi


CUHAS-BUGANDO matukio jioni-1

 Walitokelezeajeeeeeee!

CUHAS-BUGANDO matukio 4

Nimechoka kuandika angalia picha tu zinazungumza zenyewe

CUHAS-BUGANDO matukio - 3


CUHAS-BUGANGO matukio 2

Ilikuwa ni Shedaaaaa.
HONGERENI SANA (watoto wa baba paroko)

 Kuku aliye karibia kuwatoa roho wanafunzi... maana ilikuwa ukimkamata wakooooo, watu walisha nunua vitunguu ilikuwa shedaaa
 Kuku kuku kuku

CUHAS -BUGANDO matukio



KWANZA KABISA  NAPENDA  KUCHUKUA  NAFASI  HII  KUWAPONGEZA  WANA TAMELASA CUHAS –BUGANDO MWANZA PAMOJA NA WADAU  WOTE  KWA  KUONESHA KUWA  HAKUNA  KINACHOSHINDIKANA PALIPO  NA  NIA MOJA. KIPEKEE  NAUPONGEZA  UONGOZI  WA  TAMELASA-CUHAS  CHINI  YA  MWENYEKITI  WA TAWI  NDUGU, ALPHONCE CHARLES
I’ M  PROUD OF  YOU  DUDES
AMBELE   ALIAH
PRESIDENT
……………………………………………………………….
Katika kuwakaribisha  wanafunzi  wa mwaka wa kwanza  wa Degree na Diploma za maabara tiba katika chuo kikuu cha CUHAS –BUGANDO wana TAMELASA wamefanya tamasha kubwa na BONANZA tar 08/11/2014 likifuatiwa na tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Gold city hapa jijini Mwanza  tafrija  hiyo  pamoja  na  mabo  mengine  iliambatana  na  tukio  kutunisha  mfuko  wa  tawi  (FUND RISING) ambapo  pesa  taslim na ahadi zilizotolewa  ziliweza  kufikia  lengo  na zaidi. Mimi mwenyewe Mr President  nilikuwepo kushuhudia maandalizi ya mwisho na jinsi walivyoendesha zoezi zima. Nitawaletea  baadhi  ya  matukio  yaliyojiri  oneni  uhondo  ilikuwa Nishedaaaa


BONANZA
Kulikuwa na michezo mbalimbali ambayo ilileta raha na kuifanya siku iwe ya kukumbukwa

1. kukuimbia na Gunia
2. Riadha mita 100
3. kufukuza kuku
4. shindano la kula
5. kufukuza kuku na 
6. mpira wa miguu
 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia Bonza hilo wengine wakisubiri muda wa mchezo wanaoupenda wapate kushiriki


Wednesday, November 5, 2014

Picha za viongozi wa TAMELASA eastern zone

 Baadhi ya viongozi wa TAMELASA wakipiga picha baada ya kumaliza mkutano wao siku ya Jumamosi 1/11/2014 kutoka kushoto ni Magdalena (makamu mwenyekiti IMTU), Eliza (katibu IMTU), Ernest (mwenyekiti MUHAS) na Magonyozi(mwenyekiti IMTU)

NTA levels na mtaala mpya



Leo hii tarehe 05/11/2014 nimetoka ofisi ya mkurugenzi mafunzo nilikuwa na maswali machache ambayo nilitaka kupewa ufafanuzi ili niweze kuelewa na niweze kuwataarifu, kujibu au kutolea ufafanuzi baadhi ya maswali ambayo nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara na wanachama leo nitafafanua jambo moja tu sababu ya muda
1.      Nilitaka kujua  kuhusiana na mtaala mpya ambao umepitishwa na unaanza kutumika kwenye vyuo vyetu vya afya za binadamu. Mtaala mpya unaanza kutumika rasmi kwa levels zote
Kabla sijaendelea zaidi ningependa niwakumbushe kidogo hizi NTA levels. NTA ni kifupisho cha maneno National Technical Award.   Levels 1,2 na 3 zinatumika  VETA na huwa zinaandikwa NVTA. Kwa kada zote za afya tunaanza na NTA level 4. Ukisoma Level  4 na 5 unapata certificate (Laboratory assistant au Clinical Assistant) ukifaulu na GPA nzuri unaruhusiwa kuendelea na NTA level 6 moja kwa moja (Ordinary Diploma)la unakwenda kazini baadae utakwenda kusoma diploma